HOSPITALI ya Benjamin Mkapa(BMH) iliyopo makao makuu jijini Dodoma, imezindua rasmi maabara ya upasuaji magonjwa ya moyo ikiwemo matundu na kuziba kwa mishipa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dk.Alphonce Chandika alisema maabara hiyo imeanza kufanya kazi na mashine inayotumika kufanya upasuaji huo imegharimu takribani Sh.Bilioni tano.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliye mbele) akizindua rasmi maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya moyo (Cathlab) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Source: http://bmh.or.tz/2019/02/13/hospitali-ya-benjamin-mkapabmh